Yanga wanapata sare dhidi ya JKT pale Isamuyo leo.. Wanadondosha alama mbili.. Kwenye Uwanja ule mgumu wala haishangazi.. Hakukua na ufundi wala ujuzi.. Yeyote angeweza tu kufungwa
ISHU YA DRESSING ROOM IKO HIVI Simba na Yanga wote hawajatumia vyumba vya kubadilishia nguo kwa madai hewa ni nzito.. Hakuna aliyeingia vyumbani.. Hakuna aliyeingia kupitia mlango rasmi..
Wakati tukiendelea kuamini Ihefu ni timu tishio mzunguko wa Pili wa Ligi.. Imeshinda mechi MOJA tu kati ya SABA za mwisho.. Imepokea vipigo vitatu na sare tatu.. Kunani Ihefu SC?
Azam FC imecheza mechi 16 za Ligi Kuu bila kupoteza.. Ikiwemo mechi kubwa dhidi ya Yanga na Simba.. Na hapo wana majeruhi kibao.. Dube kagoma na hawana straika.. Kuna kitu huyu Mwamba anakisuka pale Chamazi.. Msimu ujao wanaweza kuwashangaza wengi
Stephane Aziz Ki.. Aliwafunga Simba akiwa na ASEC.. Amewafunga mara mbili akiwa na Yanga.. Kwa sasa ndiye kinara wa Magoli Ligi Kuu.. Mchezaji wa kuchungwa sana huyu
'Yanga tunaitazama Simba kama timu yenye viongozi makini, ukiniambia nitaje viongozi makini kwenye ligi, Simba siwezi kuwaacha, wanauzoefu na mipango ya kushinda mechi,' @alikamwe Meneja Habari na Mawasiliano Yanga Sc
Simba dhidi ya Ihefu SC leo.. Mechi muhimu sana kwa Mnyama kabla ya Dabi ya Kariakoo.. Ihefu ni wagumu kweli.. Ila Mnyama anatakiwa kushinda ili aende kwenye Dabi akiwa na morali na hali ya kujiamini zaidi.
DABI YA KARIAKOO.. Hii mechi imebeba hatma ya ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.. Yanga akishinda anajihakikishia ubingwa.. Simba akishinda anafufua matumaini ya ubingwa…