Soba (@s_soba) 's Twitter Profile
Soba

@s_soba

Attorney| Entrepreneur & a Patron~Die Hard Fan of Yanga🇹🇿

ID: 1599231901

calendar_today16-07-2013 20:26:09

9,9K Tweet

929 Followers

619 Following

Soba (@s_soba) 's Twitter Profile Photo

#NenoLaLeo Ukiwa Mawindoni, katika pori lenye swala wengi, hakikisha unalenga vema kwenye uelekeo wa swala unaemhitaji. Usifyatue risasi ovyo, jiongoze vema, risasi ni chache usizipoteze Funzo “Mtumie vizuri mtu anaeweza kukusaidia, usimtumie ovyo/vibaya” Tafakari ✍🏾

Soba (@s_soba) 's Twitter Profile Photo

#NenoLaLeo “Unapozika hadithi za masuala yaliyotokea maishani mwako kipindi kilichopita, jiepushe kukutana na wenye kulijua kaburi la hadithi hizo” ~Dkt. D. Marandu Soma tena #Tafakari✍🏾✍🏾✍🏾

Soba (@s_soba) 's Twitter Profile Photo

#NenoLaLeo Kwa kawaida wanaume huwa hawaelezi shida zao, huwa wanateseka kimya kimya. Ukiona mwanaume mwenzako anakueleza shida zake ujue wewe ni tumaini lake la mwisho, ukiwa na nafasi MSAIDIE, USIMWANGUSHE ~Dr. D. Marandu #Tafakuri✍🏾

Soba (@s_soba) 's Twitter Profile Photo

#NenoLaLeo “Kwa utimamu, utulivu na amani ya nafsi yako, usijaribishe kuelewa kila kitu” ~ Dkt. D. Marandu Soma tena 👆🏾 #Tafakuri✍🏾✍🏾✍🏾

Soba (@s_soba) 's Twitter Profile Photo

#NenoLaLeo “Ukishakua mvuvi usiogope bahari, yakija mawimbi, upepo mkali au ghasia za baharini uwe tayari kukabiliana nazo” Kuwa tayari kukabiliana na changamoto unazokumbana nazo katika harakati za maisha. Usiwe mnyonge, pambana, usikate tamaa. #Tafakuri✍🏾✍🏾✍🏾

Soba (@s_soba) 's Twitter Profile Photo

#NenoLaLeo “A” akikuunganisha na LINE au NETWORK yake anataka mfanikiwe kwa pamoja. Sio uungwana kwenda kufanya biashara na LINE au NETWORK hiyo bila “A” kufahamu tena unadiriki kumfahamisha usimwambie “A”. Jiulize “A” akijua atakufikiriaje? UAMINIFU NI UTU #Tafakari✍🏾✍🏾✍🏾

Soba (@s_soba) 's Twitter Profile Photo

#NenoLaLeo “Mtu akitambulishwa kwako na “A” ili mshirikiane katika kazi fulani, halafu baadae mtu huyo akaongeza kazi nyingine na akakwambia usimwambie “A”, achana na huyo mtu, kama hawezi kuwa MWAMINIFU (Loyal) kwa “A”, hawezi kuwa MWAMINIFU kwako #UAMINIFU NI UTU #Tafakari

Soba (@s_soba) 's Twitter Profile Photo

#MojaYaLeo_NaSSH Ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia iliyobebwa na Dkt. Samia Suluhu ili kuokoa afya ya kila mmoja wetu na kutunza Mazingira yetu imepelekea kufanyika kwa Mkutano Mkubwa Wa Wakuu wa Nchi 25 barani Afrika hapa Dar ea Salaam kuieneza Afrika nzima. Pongezi sana #SSH

#MojaYaLeo_NaSSH

Ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia iliyobebwa na Dkt. <a href="/SuluhuSamia/">Samia Suluhu</a> ili kuokoa afya ya kila mmoja wetu na kutunza Mazingira yetu imepelekea kufanyika kwa Mkutano Mkubwa Wa Wakuu wa Nchi 25 barani Afrika hapa Dar ea Salaam kuieneza Afrika nzima. Pongezi sana #SSH
Soba (@s_soba) 's Twitter Profile Photo

#TodaysThoughts Professional work, attracts professional invoice. Experts’service include; 1. Time 2. Professional Inputs/Opinion/Guidance 3. Execution/Performance/Delivery Each of the above categorically bear its value. If any or all is furnished, please PAY accordingly.

Soba (@s_soba) 's Twitter Profile Photo

#NenoLaLeo Huduma ya Kitaalamu inaenda sanjari na Malipo ya Huduma hiyo Huduma ya Kitaalamu (mf: kutoka kwa Mawakili) inahusisha 1. Muda 2. Ushauri wa Kitaalamu 3. Utekelezaji/Ufanikishaji wa huduma Kila mojawapo ina thamani yake. Ukihudumiwa kimoja au vyote TAFADHALI LIPIA.

Soba (@s_soba) 's Twitter Profile Photo

#NenoLaLeo #Jali_Muda_Wa_Mtu Ukipata nafasi ya kuchat kwa sms na kiongozi, usitumie muda mwingi kumueleza mambo tofauti na lile mahsusi unalotaka kumshirikisha, viongozi wengi hawana muda mwingi wa kuongea kila kitu #Muda_Ni_Mali

Soba (@s_soba) 's Twitter Profile Photo

#Neno_La_Leo #Jali_Hisia_Za_Mtu Muhimu sana kujua hisia au hali ya mtu kabla hujamshirikisha jambo lako. Tafakari kwanza kabla hujamshirikisha jambo lako mtu Mwenye Njaa, mwenye hasira, au anaepitia changamoto fulani. Jali kwanza hisia au hali yake kisha mshirikishe la kwako.

Soba (@s_soba) 's Twitter Profile Photo

#Neno_La_Leo #Heshima_Ni_Mali Ikitokea upo katika mazingira ya kuchagua kati ya Heshima na Pesa, basi chagua Heshima. Pesa ikiondoka inaweza kurudi. Heshima ikiondoka haiwezi kurudi. Tunza Heshima yako ufurahie Maisha yako. #Pesa_Ni_Kitu #Heshima_Ni_Utu

Soba (@s_soba) 's Twitter Profile Photo

#NenoLaLeo #Uwekezaji “Mafanikio ya Uwekezaji mzuri hudhihirika na kutamalaki iwapo utafanyika kwa watu. Wekeza kwa kuibua, kuinua, kuchochea ukuaji wa Ustawi wa Maisha ya Watu. Wekeza kwa kujenga mahusiano mazuri na watu. Uwekezaji wa namna hii hulipa maradufu” Wema Hauozi

Soba (@s_soba) 's Twitter Profile Photo

Safari ya Maisha ni Hatua, Muhimu kuzingatia Hatua zinatofautiana. Kamwe usilinganishe Hatua zako na za mwingine. Ukijifananisha utajiongoza vibaya, utajidanganya, utatengeneza husda na chuki. Heshimu na Ridhika na Hatua Zako, huyu ndio wewe🙏🏾 #AsanteKwa2025 #HeriYaMwakaMpya2026

Soba (@s_soba) 's Twitter Profile Photo

#NenoLaLeo Heri ya Siku ya Wanawake Duniani kwa wanawake wote 👏🏾 Tunawapenda ✅ Tunawathamini✅ Tunawajali✅ Tunawaheshimu✅ Tunatambua mchango wenu kwetu✅ Kwa Mwezi huu wa ibada, tunatumia muda wetu kuwaombea mafanikio mzidi kuilea, kuitunza na kuihifadhi Jamii🤲🏾

Soba (@s_soba) 's Twitter Profile Photo

#NenoLaLeo #Tubadilike “Vijana wanalalamika sio kwamba hawapendi kuwashirikisha matatizo yao, ila mnawatangaza, mnatumia shida zao kutoa mifano kama ya watu walioshindwa au kufeli maisha. Tukumbuke kuteleza sio kuanguka”. Shida za watu sio matangazo, tubadilike.

Soba (@s_soba) 's Twitter Profile Photo

#NenoLaLeo Tukisherehekea SIKU YA FURAHA ULIMWENGUNI Leo, tujitahidi sana kufanya vitu vinavyotupa furaha. 1. Kaa na watu wanaokupa furaha 2. Sikiliza vitu vizuri vya maana vinavyokupa furaha 3. Angalia vitu vizuri vya maana vinavyokupa furaha 4. Usipoteze muda kwa vitu vibaya

Soba (@s_soba) 's Twitter Profile Photo

#NenoLaLeo “Nyongeza ni sehemu ya fungu. Usiponunua huongezewi” by Hilary Mtuta (Ukiwa mwema, utalipwa wema, ukiwa mbaya je? Tafakari

Soba (@s_soba) 's Twitter Profile Photo

#NenoLaLeo Usichukie mapito magumu unayokumbana nayo maishani mwako. Nanasi ni tamu, limewekwa katikati ya miba. Asali ni tamu imewekwa katikati ya kundi la nyuki. Nyakati ngumu ni fursa, mapito tunayopita ni fursa…Tusikate tamaa ✍🏾✍🏾✍🏾