Kijana mwenzangu usidharau mafanikio yako hata kama ni kidogo kiasi gani. Kesho yako kubwa na ya ndoto zako inaanza kujengwa na kidogo ulichonacho sasa. Tena usiruhusu watu wadharau ulichonacho, kwani hawakuwepo wakati unatokwa jasho kukitafuta. Pambana amini kesho yako ni kubwa.
Ukikata tamaa, unaonesha hukuwahi kuwa na nia ya dhati. Komaa, vumilia, pigania mpaka kieleweke — ndoto hazijengwi kwa urahisi bali kwa ujasiri na uthubutu!
Sio kila kufanikiwa "being successful" kutakufanya kuwa wa maana "being significant". Unakuwa wa maana pale unapokuwa na mchango chanya kwenye maisha ya wengine. Wengi tunakiu ya majina makubwa na ukwasi lakini jamii haioni chochote cha maana kwetu. Huo nao ni ulofa #ChrisMauki
Mapito, dhoruba na vikwazo havinabudi kuja na vitasumbua sana ndoa au mahusiano yenu lakini kama mizizi yenu imeenda chini na imeshikana ardhini basi matawi na majani ndio vitatikisika ila shina liko wima. Watadhani hamfiki, mwisho wanatamani kuja mliko #ChrisMauki
Mwanaume kuna wakati utalazimika kusimama peke yako. Lakini usifanye hivyo kwa sababu ya kiburi au ukaidi.
Ikiwa unahitaji msaada, omba msaada. Ukiona mwanaume mwenzio anahitaji msaada. Simama naye. Mtendee vile ambavyo ungetamani kutendewa.
Wengi wetu tuna pupa ya kutaka kubadili mazingira yetu na kuwabadili wanao tuzunguka ila ni ngumu sana sisi kubadilika. Hapo ndipo wengi tunakwama #ChrisMauki
Hao ndugu na marafiki zako wanao kuaminisha kwamba bila wewe hawawezi maisha. Wanakutegemea wewe kwenye kila kitu. Na wewe una stress kila siku kuwawaza wao. Nakwambia siku ukifa bado wataishi fresh tu. Usimfie asiye tayari kujifia #ChrisMauki
USIANZE BIASHARA KAMA HUJUI HAYA MAMBO
Mambo 10 Niliyotamani Kujua Mapema Kabla Sijaanza Biashara
Shuka nayo 👇🏾 uzi 🧵
1. Biashara sio njia ya haraka kuwa tajiri Inahitaji muda, juhudi na subira kubwa
2. Mauzo hayawezi kuwa makubwa kila siku • lazima uvumilie.
Mfanyabiashara anayetaka kufanikiwa lazima awe na ujuzi wa kifedha ktk haya:
1. Kuweka kumbukumbu za mapato/matumizi/faida
2. Kupanga matumizi kulingana na mapato
3. Kutofautisha mapato na faida
4. Kuweka akiba na kuwekeza faida
5. Kuelewa gharama za uendeshaji
6. Uelewa wa kodi