1. Tulifika Mkoa wa Manyara asubuhi saa 4.30 kwa lengo la kuwa tembelea wahanga wa mafuriko waliopoteza ndugu, waliopo hospitali na waliopo makambini. Aidha, tulikusudia kujionea wenyewe uharibifu wa mali na miundombinu ili nasi tuone njia bora ya kusaidiana na wadau wengine