Kigwa Aveki
@avekikigwa
Agriculture Advisor||Farmer||Organic farming Specialist||Manchester united & Simba SC die hard fan
ID: 1224219675376136192
03-02-2020 06:35:05
6,6K Tweet
775 Followers
209 Following
Kwenye maonyesho ya kilimo Mwaka huu TARI Tanzania official page nilikutana na aina ya mbegu ya mtama ambao hauliwi na ndege π Ni vile sikutaka kuuwekea maanani tu.
Je wajua Ulaji wa mahindi wa nyani, ngedere na Fungo ni tofauti. Nyani na Ngedere hula mchana wakati Fungo hula usiku. Ukifika shamba asubuhi ukatuta mahindi yameliwa basi ujue Fungo huyo. Wako Kigwa Aveki
Hulka ya vijana wengi kukimbia kilimo na kuwaachia wazee inasababisha ujuzi, uzoefu na teknolojia bora za zamani kupotea wazee wanapofariki. Kazi kwetu vijana Wako Kigwa Aveki
Upotevu wa Mazao makuu ya nafaka nchini ~Mahindi 15.5% ~Mpunga 10.7% ~Matama 12.5% Bado juhudi za ziada inabidi kufanyika kiwango hiko ni kikubwa sana. Wako Kigwa Aveki
Kutokana na lishe duni hupelekea 53% ya wajawazito nchini Tanzania kuwa na upungufu wa damu Sekta ya kilimo tunakazi ya kufanya lakini hata kama tukizalisha kwa wingi bila ya vipato mfukoni bado changamoto itabaki pale pale. Tutazalisha watashindwa kununua π Wako Kigwa Aveki
Kwa mwaka tunazalisha mahindi zaidi ya tani milioni 7 kwa kuogopa ushindani wa kibiashara huko walikosaini mikataba wakaweka vizuizi viiiingi mwisho wa siku wameshindwa kinunua mzigo wote watu wanalia bei haiongezeki π Wako Kigwa Aveki
Je wajua Ukitumia kiuagugu chenye FORMESAFAN na IMAZETHAPYR kwa ajili ya kuzuia magugu kwenye Soya na Karanga msimu unaofata kwenye shamba hilo hilo ukipanda mahindi hayatofanya vizuri. Usije sema umerogwa Wako Kigwa Aveki
Kuna siku tulikuwa na mjadala mkali sana kuhusu kuoza kitako (Brossom end rot) na kutumia booster au mbolea yenye Calcium. Ripoti kutoka vyuo vya kilimo (India na USA) wanaandika ili kuzuia tatizo weka mbolea yanye Calcium wiki 1 baada ya tunda kutengenezwa Wako Kigwa Aveki
Usimamizi mzuri wa visumbufu vya mazao hauongezi uwezo wa mazao kutoa mavuno mengi. Ila inasaidia kupunguza upotevu wa Mazao π. Wako Kigwa Aveki
Mkulima kunde zake zimeshambuliwa na aphids anataka anunue kiuatilifu elfu 5 nilimwambia asininue aache tu. Kitu wakulima wengi hawafahamu "VIUATILIFU VINAHITAJI PESA KADRI UTUMIAVYO KWA WINGI NDIVYO PESA INAZIDI KUTUMIKA NA NDIO FAIDA HUZIDI KUPUNGUA" π Wako Kigwa Aveki