Marcely Kanoni. (@ckmarcely) 's Twitter Profile
Marcely Kanoni.

@ckmarcely

Husband, Legal Counsel - Advocate of the High Court of Tanzania, Roman Catholic, Manchester United fan.

ID: 1145025050476765184

calendar_today29-06-2019 17:43:40

176 Tweet

61 Takipçi

257 Takip Edilen

Marcely Kanoni. (@ckmarcely) 's Twitter Profile Photo

Ulinisukuma sana ili nianguke; Lakini Bwana akanisaidia. Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu, Naye amekuwa wokovu wangu. Sauti ya furaha na wokovu, Imo hemani mwao wenye haki. 🎼🎼Mshukuru Bwana kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake ni za milele.🎼🎼 #Dominika

Marcely Kanoni. (@ckmarcely) 's Twitter Profile Photo

Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako. Hos. 4:6.

Marcely Kanoni. (@ckmarcely) 's Twitter Profile Photo

Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana? Au ni nani aliyekuwa mshauri wake? Au ni nani aliyempa yeye kitu kwanza, naye atalipwa tena? Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amina. #DOMINIKA

Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana? Au ni nani aliyekuwa mshauri wake? Au ni nani aliyempa yeye kitu kwanza, naye atalipwa tena? Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amina.

#DOMINIKA
Marcely Kanoni. (@ckmarcely) 's Twitter Profile Photo

Lakini sasa, Ee Bwana, wewe u baba yetu; sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu kazi ya mikono yako. #DominikaYaKwanzaYaMajilio🙏🏽 #NikoTayariKwaMwanza2024 #KaaNasiMungu

Lakini sasa, Ee Bwana, wewe u baba yetu; sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu kazi ya mikono yako.

#DominikaYaKwanzaYaMajilio🙏🏽
#NikoTayariKwaMwanza2024
#KaaNasiMungu
Marcely Kanoni. (@ckmarcely) 's Twitter Profile Photo

Bwana akubarikie, na kukulinda; Bwana akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili; Bwana akuinulie uso wake, na kukupa amani. [Hes 6:22-27] #ThankYouMyAlmightyGod #HappyNewYear2024.

Marcely Kanoni. (@ckmarcely) 's Twitter Profile Photo

Hekima ameijenga nyumba yake, amezichonga nguzo zake saba; Amechinja nyama zake, amechanganya divai yake, ameiandalia meza yake pia. Kila aliye mjinga na aingie humu, tena anamwambia mtu aliyepungukiwa na akili, njoo ule mkate wangu, ukanywe divai niliyoichanganya. #Mit 9: 1-6.

Marcely Kanoni. (@ckmarcely) 's Twitter Profile Photo

Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao ?. #Yak 2:5

Pope Francis (@pontifex) 's Twitter Profile Photo

The Word of God repeats to us, as to Bartimaeus: “Take heart; get up, He is calling you.” Let us throw off the cloak of apathy and entrust our blindness to the Lord. Let us stand and carry the joy of the Gospel through the streets of the world. #GospelOfTheDay

Marcely Kanoni. (@ckmarcely) 's Twitter Profile Photo

Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamuona kama alivyo. Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa; kama yeye alivyo mtakatifu. #WatakatifuWote #Mtuombee!

Marcely Kanoni. (@ckmarcely) 's Twitter Profile Photo

Roho zao wenye haki wamo mkononi mwa Mungu,wala maumivu hayatawagusa. Machoni pa watu walio wajinga walionekana wamekufa,na kufariki kwao kulidhaniwa kuwa ni hasara yao,na kusafiri kwao kutoka kwetu kuwa ni uharibifu wao;bali wao wenyewe wamo katika amani #KuwaombeaMarehemuWote

Marcely Kanoni. (@ckmarcely) 's Twitter Profile Photo

Mwanangu umsaidie baba yako katika uzee wake; wala usipate kumhuzunisha siku zote za maisha yake. Akiwa amepungukiwa na ufahamu umwie kwa upole, wala usimdharau iwapo wewe u mzima sana; kwa maana sadaka apewayo baba haitasahauliwa. [YbS 3:2-6, 12-14] #FamiliaTakatifu

Marcely Kanoni. (@ckmarcely) 's Twitter Profile Photo

Bwana akubarikie, na kukulinda; Bwana akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili; Bwana akuinulie uso wake, na kukupa amani. [Hes 6:22-27] #ThankYouMyAlmightyGod #HappyNewYear2025.

Marcely Kanoni. (@ckmarcely) 's Twitter Profile Photo

Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji,akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo? Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli. [1 Yoh 3:17-18] #MioyoYetuIjaeUpendoUsiokuwaNaMipaka.

Alexander (@alesandrojr) 's Twitter Profile Photo

"Kanisa ni Takatifu, sio kwa sababu ya matendo yetu, bali kwa sababu kichwa chake ni Kristo mwenyewe ambaye ni Mtakatifu. Kazi yetu sisi ni kuishi kwa kumfuata Yeye, sio kuunda Kanisa kwa mfano wetu" ~ Papa Leo XIV

"Kanisa ni Takatifu, sio kwa sababu ya matendo yetu, bali kwa sababu kichwa chake ni Kristo mwenyewe ambaye ni Mtakatifu. Kazi yetu sisi ni kuishi kwa kumfuata Yeye, sio kuunda Kanisa kwa mfano wetu" ~ Papa Leo XIV
Marcely Kanoni. (@ckmarcely) 's Twitter Profile Photo

Tazama, Mungu hatamtupa mtu mkamilifu, Wala hatawathibitisha watendao uovu. Bado atakijaza kinywa chako kicheko, Na midomo yako ataijaza shangwe. Hao wakuchukiao watavikwa aibu; Nayo hema yake mwovu haitakuwako tena. Ayubu 8:20-22.

Marcely Kanoni. (@ckmarcely) 's Twitter Profile Photo

Ilipotimia siku ya Pentekoste….Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi zilizogawanyika, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu. Mdo 2:1-4.

Marcely Kanoni. (@ckmarcely) 's Twitter Profile Photo

Mwanangu, wakati wa kufanikiwa uendelee katika unyenyekevu; hivyo utapendwa kuliko mwenye ukarimu. Kadiri ulivyo mkuu uzidi kujinyenyekesha, nawe utapata kibali machoni pa Bwana; kwa maana rehema zake Bwana zi kuu, na siri yake ni kwa wanyenyekevu. [YbS 3:17-20]

Marcely Kanoni. (@ckmarcely) 's Twitter Profile Photo

Mimi ni wa Paulo, na,Mimi ni wa Apolo, na , mimi ni wa Kefa, na, Mimi ni wa Kristo. Je, Kristo amegawanyika? Je Paulo alisulibiwa kwa ajili yenu? Au je, mlibatizwa kwa jina la Paulo? Maana Kristo hakunituma nibatize, bali niihubiri Habari njema. [1 Kor 1: 12-13, 17]. #DOMINIKA

Marcely Kanoni. (@ckmarcely) 's Twitter Profile Photo

Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima….Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni. [Mt 5: 14, 16] #DOMINIKA

Marcely Kanoni. (@ckmarcely) 's Twitter Profile Photo

Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye…Kwa maana alisema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nilikusaidia; tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa. #JUMATANOYAMAJIVU