KELELE ZA KUTEKWA RAIA TANZANIA ZINAONGEZEKA. Leo mke wa Abdallah Muna amesema: Mume wangu tarehe 31.1.24, (aliripoti Polisi Arusha)”. “Baada ya kutoka kuna watu walimfuatilia”. “Toka siku hiyo (ametekwa), hajapatikana tena”. KAMA WANAOTEKWA NI WAHALIFU WAPELEKWE MAHAKAMANI.
MAUWAJI ya kiholele yanakomaa nchini kwetu. Ni yale ya kutekwa na kupotezwa au kupatikana Maiti kwa utata. Watekaji huwa na Magari, Redio, Silaha pia hujitambulisha ni Usalama. Kwa hali hiyo Raia wanapo tuhumu, wazingatiwe badala ya kutishwa. Uhai ni kitu kibwa si cha kuchezewa.
SALAMU: 1. Muungano haukupata ridhaa ya Wananchi. Si sawa kutoa kafara mataifa yetu kwa sababu ya Muungano wa Viongozi 2. Inasemwa Kero zimekwisha, haziwezi kwisha bila makubaliano halali na Katiba ya Serikali 3. 3. Matokeo, miaka 60 sasa serikali zote 2 na raia ni maskini sana.
Si sahihi kutukanwa Raia au Kiongozi. Lakini mazingira yanaonesha CCM NDIO MWALIMU WA MATUSI KWA VIONGOZI. Moja ya ushahidi ni SAUTI YA KISONGE. Kwa miaka mingi imefurika matusi kwa Maalim Seif Sharif Hamad. Waandishi na Wahariri wa Kisonge hawajatekwa wala kupotezwa.
Toka 2013-2024, watu wanatekwa na kupotezwa. 2023, Shura ya Maimamu ilitoa ripoti ya uchunguzi. Katika ripoti hiyo jumla raia 236, wametekwa na kupotezwa. Kauli ya CCM “HAWA TUKIWAPOTEZA MSIWATAFUTE” inawafanya watuhumiwa Na.1. Kama taifa linajali uhai wa raia Dola ichukue hatua.
Wagonjwa wa figo wanatozwa Sh. 400,000/600,000, kila juma katika hospitali za Serikali. Tungenunua magari ya kawaida, mapesa yatakayobaki yangenunua mashine za kutosha wagonjwa wakasafishwa figo bure kama Komoro. Si sawa kununua magari ya kifahari wakati hospitali hazina uwezo.
“Mwanangu hajaugua wamemuuwa”. “Mama Samia wewe ni mzazi, mtoto anauma”. Hayo ni malalamiko ya mzazi ambaye mwanaye kafa mikononi mwa Polisi Karatu. Msiba mkubwa Tanzania ni pale raia wanapolalamika uvunjwaji wa haki za msingi lakini viongozi hawajali wala kuzuwia matukio hayo.
Polisi TZ wamekiri kumshikilia Imamu Yasin. Pia wamekiri utekwaji raia upo ila wao hawahusiki na waliotekwa na kupotea kabisa. Lakini utaratibu walioutumia kumchukua imamu ndio huo huo uliotumika kwa mamia ya raia waliopotea kabisa. Katika hali hii mtuhumiwa wa utekaji ni nani?
Utekwaji wa raia Tanzania unaongezeka: Trh 5/7/23 katekwa Aflah Nawanda (Dar). Trh 7/2/24 katekwa Imam Shaaban Khamisi (Magole Dar). Trh 13/3/24 katekwa Imam Abdurahman (Geita). Anayetekwa Tanzania maana yake kaondolewa duniani. Ni kweli Serikali haiwajui wanaoteka raia?
Tumepeleka Congratulation kwa Balozi wa Afrika Kusini. Sehemu ya Waraka inasema “Ingawa hukumu ya Mahakama ya Kimataifa haijatoka lakini tayari mmeshinda katika Mahakama ya Ubinadamu na Mahakama ya maoni ya watu. Kitendo chenu kimegusa nyoyo na akili za mamilioni ya watu duniani”
Rais wetu shughulikia Uhai wa Raia. Trh. 27.12.23, Polisi wamewauwa Bakari Ismail na Shomari Kacheuka. Trh. 28.12.23 kikosi cha Utekaji kimewateka Juma Idd na Haruna Idd. Matukio haya na hukumu za kunyongwa watu yanakithiri katika Serikali yako. Siasa sawa lakini Uhai ndio Na.1.
MASHEIKH WENGINE 5 WAFUNGWA ARUSHA LEO. Sinema hii inaonesha awamu ya 4 na ya 5, zilikuwa na jukumu la kuwakamata Masheikh (na baadhi kuwapoteza) na awamu hii inatekeleza jukumu la kuwafunga na hukumu za kunyonga. Leo Mahakama Kuu Arusha imewahukumu Masheikh wengine 5, miaka 30.
TANZANIA TAIFA LISILO JALI MAADILI. Huteuwa viongozi wasio na Maadili. Baadhi hupewa mamlaka nyeti kama za kutunga Sera. Zanzibar imemualika Shoga R. Quest kutoka Ulaya akuze Utalii. Swali, ikiwa atawashauri waimarishe Ushoga kama njia ya kukuza Utalii watapinga?
MSHEIKH 6 WAHUKUMIWA KUNYONGWA LEO ARUSHA. Wawili waachiwa huru. Ni sehemu ya mamia ya Waislamu wanao tuhumiwa na Serikali kwa Ugaidi. Wamekaa gerezani miaka 10. Wengine 10, wamekwisha hukumiwa kunyongwa Tanga. Awamu ya 4 na ya 5 waliwakama, awamu ya 6 inafunga na kuwanyonga.
“Malengo makubwa ni 3: Kwanza kudai Tume Huru ya Uchaguzi pili nyumba za Serikali zilizouzwa zirudishwe na tatu mgao wa haki katika mikataba ya Madini”. Makala yenye wito huo yalitolewa na Prof. Safari 2005. TUUNDE TUME HURU ili tupate Madiwani, Wabunge nk kwa ridhaa ya Wananchi
TUMEFANYA ZIARA MAGEREZA 3: TRH 2/9/23 Isanga Dodoma: Wapo Waislam 6 wamefungwa miaka 50 kwa madai ya kutaka kupindua Serikali. TRH 3/9/23 Gereza la Arusha: Masheikh 12 mahbusu kwa miaka 9.
TRH 4/9/23 Gereza la Tanga: Wapo Masheikh 10 walio hukumiwa kunyongwa kwa madai ya Ugaidi
TUTOE ZAKA: 1. Zaka inasafisha kipato. 2. Inaondoa husda na kuleta mapenzi kwa mpokeaji. 3. Inaongeza ajira na mzunguko wa fedha. 4. Mtu au jamii ambayo haitoi zaka inaondolewa baraka badala yake watapata dhiki na shida mbalimbali. TUTOE ZAKA.