Cap. 3 R.E 2023 - Basic Rights and Duties Enforcement Act - Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Msingi na Majukumu. Katiba imetoa Haki za Msingi na Majukumu/Wajibu mbalimbali, sasa endapo Katiba itakiukwa, hii Sheria inakupa utaratibu wa kufuata ili kudai Haki za Msingi za ππ½ππΌ
Cap. 4 R.E 2023 - Laws Revision Act - Sheria ya Urekebu [Marekebisho] wa Sheria: Uandaaji, uchapishaji, urekebishaji endelevu, utunzaji nk wa Sheria, unasimamiwa na hii Sheria
Mf. Sheria ambazo zimesambaratika, zinaletwa pamoja kwenye Nyumba moja - Kitabu kimoja. Yaani ππΌ
Cap. 5 R.E 2023 - Government Proceedings Act - Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Serikali, Sura ya 5. Unataka kuishtaki Serikali? Au Serikali imekushtaki na wewe unataka kuweka Madai Kinzani - Counter Claim? Hii ndio Sheria inakupa utaratibu wa namna ya kufanya.
kitu kinakera ππΌ
Cap. 6 R.E 2023 - Evidence Act - Sheria ya Ushahidi, Sura ya 6. Inajieleza yenyewe, mambo hayusuyo Ushahidi Mahakamani, yametulia kwa hii Sheria. Lakini kumbuka hii Sheria haitumiki kwenye mambo ya Ushahidi unaokuja kwa njia ya Kiapo - Affidavit. Mahakama ya Rufani ilisema ππΌππ½
Cap. 8 R.E 2023 - Reciprocal Enforcement of Foreign Judgements Act - Sheria ya Utekelezaji Sawia wa Hukumu za Mamlaka za Nchi za Kigeni, Sura ya 8. Ni Sheria inahusu utekelezaji wa Hukumu kati ya Tanzania Bara na Nchi zingine ambazo Tanzania imeingia ππΌππ½
Cap. 9 R.E 2023 - Presidential Affairs Act - Sheria ya Masuala ya Ofisi ya Rais, Sura ya 9. Inahusu masuala yahusuyo Kazi na Ofisi ya Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu. Inakuelekeza ufanyeje ukitaka kumshtaki Rais yeye Binafsi - Personal Capacity, Mshtaki baada ya ππ½ππΌ
Cap. 11 R.E 2023 - Magistratesβ Courts Act - Sheria ya Mahakama za Mahakimu, Sura ya 11. Ni Sheria ya inatoa mamlaka, nguvu na kazi za Mahakama za Mahakimu pamoja na mambo mengine yanayohusiana na hayo.
Ni moja kati ya Sheria muhimu na inayotumika sana Mahakamani. Mahakama ya ππΌ
Cap. 12 R.E 2023 - Notaries Public and Commissioners for Oaths Act - Sheria ya Wathibitishaji Nyaraka na Makamishna wa Viapo, Sura ya 12. Unataka kuithibitisha (Certify) Nyaraka yako, unataka kupata Kiapo nk, hii Sheria imekutajia watu wanaoweza kukufanyia hivyo na namna ππ½ππΌ
Cap. 13 R.E 2023 - Law of the Child Act - Sheria ya Mtoto, Sura ya 13. Inajumuisha Sheria zinazohusiana na Watoto, inataja Haki za Mtoto, kumtunza, kumlinda na kudumisha ustawi wa Mtoto kwa lengo la kutekeleza Makubaliano ya Kimataifa kuhusu Haki za Mtoto na malezi kwa ππ½
Cap. 14 R.E 2023 - Hire Purchase Act - Sheria ya Karadha, Sura ya 14. Kopa Nunua, nakuuzia kitu, utanilipa kidogo kidogo kwa awamu, nakupa kabisa hicho kitu unaondoka nacho, lakini mmiliki bado nakuwa mimi mpaka ukinilipa awamu ya mwisho - kama awamu zilikuwa 10, ukanilipa 9, ππ½
Cap. 15 - Arbitration Act - Sheria ya Usuluhishi, Sura ya 15. Inatoa mwenendo unaohusiana na usuluhishi wa ndani, usuluhishi wa kimataifa na utekelezaji wa tuzo za usuluhishi wa nje. Inafuta Sheria ya Usuluhishi ya tangu ukoloni.βπΌ
MD, Mendez (M.C.A)
08/07/2025, Day 5 Cap.15