Uchambuzi kabla ya mchezo wa leo kati ya Stellenbosch na Simba SC pale Durban, kupitia DStv (TZ) ambapo umerushwa channel namba 225 (Soccer Africa), tunamwaga yai lililochanganywa na lugha mama
UBAYAAAAA, UBWELAAAAAA
Wamefika FAINALI kwa kustahili, wamecheza mashindano haya kwa umakini mkubwa tangu mwanzo mpaka hapo walipo. Si ajabu wakirudi na Kikombe mwaka huu, uwakilishi wao kwenye ukanda wa CECAFA na Tanzania ni wa kupigia mfano.
“Tumepokea pongezi kutoka kwa raia namba 1 wa Tanzania Rais Samia Suluhu Hassan ambazo ni bora sana kwetu, tumepongezwa na wadau na taasisi mbalimbali za soka ndani na nje ya nchi, tumepongezwa na wanachama na mashabiki wetu, hatutarajii kutoka kwingine kokote” Murtaza Mangungu.
Tuna kazi ya kutofautisha WACHAMBUZI WA SOKA na Comedians! Tumefika pabaya sana kwenye uchambuzi wa mambo michezo hasa soka, eneo huru ambalo kila mmoja anatafuta kwenda mjini kwa kujaribu “Kucheksha” au kusifia wanaomfadhili. Hii ni staili mpya inaitwa UCHAMBUZI KATUNI.
YANGA SC YAANGUKIA PUA CAS
Mahakama ya usuluhishi michezoni imesema haina mamlaka ya kuzuia kupangwa kwa tarehe ya DABI kama ilivyombwa na Yanga SC huku pia ikiitaka mahakama hiyo iipe alama 3 na mabao 3, CAS pia wameitaka Yanga kupeleka kesi ya msingi TFF pia. DABI IPO PALE PALE
Bodi ya Ligi Kuu inasema itapitia ratiba ya Ligi na kutoa ratiba mpya itakayojumuisha mchezo namba 184 (Yanga Vs Simba) MAPEMA IWEZEKANAVYO.
Hii imekuja baada ya Mahakama ya Usuluhishi michezoni - CAS kuitupilia mbali kesi ya Yanga SC dhidi ya TFF, Bodi ya Ligi na Simba SC.
DABI YA KARIAKOO NI 15 JUNI,2025
Bodi ya Ligi Kuu imetoa ratiba MPYA ya kumalizia msimu wa 2024/2025 ambapo mchezo namba 184 wa Yanga Vs Simba ulioghairishwa 8 Machi,2025 na Bodi ya Ligi Kuu sasa utapigwa Juni 15,2025 Jumapili Saa 11:00 jioni pale Benjamin Mkapa.
Baada ya kusoma para ya 3 ya Taarifa kwa umma nilitegemea kusikia Yanga SC wamejiondoa kwenye Ligi na kombe la shirikisho kama kweli wamemaanisha, vinginevyo kucheza kushiriki Ligi na mamlaka unazozituhumu namna hii ni kutuongopea na kujihalalishia kuitwa Maadili kwa viongozi wao
Kwa niaba ya Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele, Mwenyekiti wa JKT Tanzania Kanali Geofrey Mvula na Mkuu wa Kikosi cha 836KJ Luteni Kanali Javan Bwai, tunashukuru sana kwa pongezi hizi kutoka kwa wadau mbalimbali wa soka nchini. Maendeleo hayana Chama
PIERRE GHISLAIN ATCHO kutoka Gabon 🇬🇦 (Pichani) atakuwa mwamuzi wa kati kwenye fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho la CAF hapo tarehe 17.05.2025 kwa mujibu wa CAF wenyewe.
BİN KAZUMARI MTIPA (The voice of the voiceless)
KWA-MKAPA INAWEZEKANA
Comeback ipo Kwa-Mkapa tena nyeupe kama tissue, ule mchecheto wa dakika 20 za mwanzo na Mpanzu leo kakojoa kitandani pia, halafu Mpanzu tangu nusu fainali ya pili pale SAUZI sio yuuuulee. Kombe hili litabaki TANZANIA 🇹🇿
Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya Wanawake STUMAI ABDALLAH (28 goals) kwenye mechi 18,kutoka JKT Queens Mabingwa wa WPL.Mwaka wetu huu tayari tuna kikombe na tunzo ya mfungaji bora. Tunasubiri
1. Best Coach
2. Best GK
3. Best Team
4. Upcoming Player
5. Youngest Player
6. Besta player