Nimesikitishwa na vifo vya watu 4 vilivyosababishwa na ajali ya treni eneo la Malolo, Tabora. Nawapa pole wafiwa, nawaombea marehemu wapumzike kwa amani na majeruhi wapone haraka. Nimeagiza tuliowapa dhamana ya eneo hili kufuatilia na kubaini chanzo, na kuchukua hatua stahiki.