Jambo FM Radio Tanzania (@jambofmtz) 's Twitter Profile
Jambo FM Radio Tanzania

@jambofmtz

The official Twitter account for Jambo FM Radio.

Habari 📢 Muziki 🎶 Burudani 🎉 #FreshiKilaSiku

Sikiliza live kwenye tovuti yetu 👇

ID: 1564829540530143262

linkhttps://jambofm.co.tz/ calendar_today31-08-2022 04:18:08

5,5K Tweet

394 Takipçi

98 Takip Edilen

Jambo FM Radio Tanzania (@jambofmtz) 's Twitter Profile Photo

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Amos Makalla amesema amerudi nyumbani kwani Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni nyumbani kwake na hivyo amekuja kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha chama tawala kinaendelea kupiga hatua kuanzia pale walipoishia wenzake.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, John Mongella amewataka Wanachama wa CCM wajiamini huku akisema kumekuwa na maeneo Wana CCM wanatishwa kitoto ambapo amewataka wasikubali kutishwa na yeyote.

Dakika 45' za kipindi cha kwanza cha mchezzo #CAFCL hakuna aliyeweza kufunga goli kwa mwenzake. Mamelodi Sundowns FC 0-0 Young Africans SC

Dakika 45' za kipindi cha kwanza cha mchezzo #CAFCL hakuna aliyeweza kufunga goli kwa mwenzake.

Mamelodi Sundowns FC 0-0 Young Africans SC
Jambo FM Radio Tanzania (@jambofmtz) 's Twitter Profile Photo

Yanga inatupwa nje kwenye michuono ya Ligi ya Mabingwa baada ya kukubali kupigwa penati 3:2 dhidi ya Mamelodi Sundowns. Hatua ya penati imekuja baada ya kutoka bila kufungana kuanzia Mchezo wa kwanza na huu wa leo wa marudiano.

Yanga inatupwa nje kwenye michuono ya Ligi ya Mabingwa baada ya kukubali kupigwa penati 3:2 dhidi ya Mamelodi Sundowns.

Hatua ya penati imekuja baada ya kutoka bila kufungana kuanzia Mchezo wa kwanza na huu wa leo wa marudiano.
Jambo FM Radio Tanzania (@jambofmtz) 's Twitter Profile Photo

Sio simba wala Al Ahly ambaye amepata goli mpaka sasa. Hata hivyo Al Ahly anagoli ambalo alimfunga simba akiwa kwao. Kama matokeo yataenda hivyi hadi mwisho basi Simba atakuwa ametolewa kwenye mashindano haya ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Sio simba wala Al Ahly ambaye amepata goli mpaka sasa. Hata hivyo Al Ahly anagoli ambalo alimfunga simba akiwa kwao.

Kama matokeo yataenda hivyi hadi mwisho basi Simba atakuwa ametolewa kwenye mashindano haya ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Jambo FM Radio Tanzania (@jambofmtz) 's Twitter Profile Photo

Msanii mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Malu Stonch amefariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa kwenye majukumu yake ya kikazi. Malu alianguka ghafla jukwaani katika ukumbi wa Target uliopo Mbezi Beach wakati akiimba pamoja na bendi yake anayofanya nayo kazi ya FM Academia.

Msanii mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Malu Stonch amefariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa kwenye majukumu yake ya kikazi.

Malu alianguka ghafla jukwaani katika ukumbi wa Target uliopo Mbezi Beach wakati akiimba pamoja na bendi yake anayofanya nayo kazi ya FM Academia.
Jambo FM Radio Tanzania (@jambofmtz) 's Twitter Profile Photo

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania imetangaza kuwa mchezo kati ya Yanga na Simba maarufu kama Kariakoo Derby utapigwa ifikapo Aprili 20 mwaka huu ndani ya dimba la Mkapa majira ya saa 11:00 Jioni

Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limethibitisha kuwakamata watu 17 raia kutoka nchini Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini bila ya kufuata utaratibu ikiwemo kutokuwa na vibali.

Watu zaidi ya 90 wamepoteza maisha nchini Msumbiji, baada ya boti waliyokuwa wanasafiria kuzama hapo jana kwenye mkoa wa Nampula, wakielekea katika kisiwa kilichoko karibu na mji wa Lumbo.

Aliyekuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo ambaye kwa sasa ni RC mpya wa Arusha, Paul Makonda tayari amepokelewa Jijini Arusha mapema leo hii anarajiwa kukabidhiwa Ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Ndg. John Mongella ambaye kwasasa ni Naibu Katibu Mkuu CCM.

Rapa kutoka Marekani, J. Cole amemuomba radhi rapa Kendrick Lamar kwa kum-diss kwenye ‘7 Minute Drill”. J. Cole alilazimika kukatiza kutumbuiza kwenye onyesho lake kwenye Tamasha la Dreamville la 2024 huko North Carolina siku ya jana Jumapili ili kumwomba Lamar msamaha.

Rapa kutoka Marekani, J. Cole amemuomba radhi rapa Kendrick Lamar kwa kum-diss kwenye ‘7 Minute Drill”.

J. Cole alilazimika kukatiza kutumbuiza kwenye onyesho lake kwenye Tamasha la Dreamville la 2024 huko North Carolina siku ya  jana Jumapili ili kumwomba Lamar msamaha.
Jambo FM Radio Tanzania (@jambofmtz) 's Twitter Profile Photo

Bondia matata Kanda ya Ziwa kutoka Manispaa ya Kahama, Shinyanga, Issa Salum James [Issa Simba], amepanda viwango na kuwa bondia namba pili Tanzania kwenye uzito wa Super lightweight, nyuma ya kinara Tony Rashid wa Dar es salaam.

Kutoka Nigeria Rema aliamua kususia tamasha la Dreamville la 2024 ambalo limefanyika huko North Carolina siku ya jana Jumapili baada ya kuchukizwa udhaifu wa sauti(Sound) hivyo akaamua kuondoka jukwaani.

Mwaka wa fedha 2022/23 imetoa Sh Bil16.5 kwa ajili ya ukarabati wa Hospitali kongwe 19 ambapo kwenye mwaka wa fedha 2023/24 kiasi cha Sh Bil 27.9 kilitengwa kukarabati hospitali kongwe 31 zilzobaki ikiwemo Hospitali ya Magunga Mji wa Kongwe ambayo imetengewa Mil 900.

Mwanamuziki wa bendi ya FM Academia, Malu Stonch aliyefariki baada ya kuanguka ghafla jukwaani, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, atazikwa siku ya Jumatano katika makaburi ya Kwa Kondo yaliyopo Ununio.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu ametoa onyo kwa Mbunge wa Viti Maalum, Ester Bulaya kufuata utaratibu wa Bunge wa kuacha kuzungumza bungeni bila kibali cha spika.