Tanzania Updates ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ(@TanzaniaUpdates) 's Twitter Profileg
Tanzania Updates ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

@TanzaniaUpdates

Follow kupata updates na ripoti mbalimbali za uhakika kuhusu Tanzania.

ID:1668995452035842049

calendar_today14-06-2023 14:55:19

61 Tweets

13 Followers

18 Following

Tanzania Updates ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ(@TanzaniaUpdates) 's Twitter Profile Photo

Treni mpya ya umeme inatarajiwa kuwasili nchini jumanne Machi 26 mwaka huu tayari kwa kuanza kazi mwezi Julai.

Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi na shirika la reli nchini (TRC)

account_circle
Tanzania Updates ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ(@TanzaniaUpdates) 's Twitter Profile Photo

Waziri wa elimu,sayansi na teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa kupitia sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 toleo la mwaka 2023 ambayo imeanza kutekelezwa January 2024, wenye taaluma ya ualimu wataanza kufanyiwa tathmini ya mitihani ili kupata ajira

account_circle
Tanzania Updates ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ(@TanzaniaUpdates) 's Twitter Profile Photo

Waziri wa elimu, sayansi na teknolojia, Prof Adolf Mkenda amesema kuwa mitaala mipya imeanza mwaka huu ikihusisha ngazi ya darasa la kwanza na la tatu, upande wa sekondari imeanzia kidato cha kwanza na kidato cha tano pamoja na vyuo vya ualimu

account_circle
Tanzania Updates ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ(@TanzaniaUpdates) 's Twitter Profile Photo

Rais wa Senegal, MackySall amekubali kufanya mabadiliko ya tarehe ya uchaguzi mkuu kutoka Disemba 15, 2024 hadi Machi 24, 2024 kutokana na maandamano yanayotaka aheshimu muda wake wa kuondoka madarakani

account_circle
Tanzania Updates ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ(@TanzaniaUpdates) 's Twitter Profile Photo

Kampuni ya Asas inayohusika na usambazaji wa maziwa imetunukiwa tuzo ya heshima kwa viwango na ubora kutoka Super Brand East Africa Choice. Tuzo hizo zimetolewa jijini Dar es Salaam

account_circle
Tanzania Updates ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ(@TanzaniaUpdates) 's Twitter Profile Photo

Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Dar es salaam (DAWASA) imetoa taarifa kwa wateja wake wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha maji Ruvu chini kuwa kutakuwa na upungufu wa huduma za maji kuruhusu maboresho ya msingi kuanzia leo Jumanne jioni hadi Alhamis March 7, 2024

account_circle
Tanzania Updates ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ(@TanzaniaUpdates) 's Twitter Profile Photo

Ushirikiano wa NMB na UBX inayounganisha benki 17 kupitia mtandao wa Umoja Switch umeiwezesha benki ya NMB kuunganisha benki 17 kwenye mtandao wake wa ATM lengo likiwa kuongeza wigo wa upatikanaji wa mashine za ATM na kupunguza gharama za miamala ya ATM kwa wateja wa benki.

account_circle
Tanzania Updates ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ(@TanzaniaUpdates) 's Twitter Profile Photo

Baraza la sanaa,sensa,filamu na utamaduni la Zanzibar (BASSFU) limemfungia msanii wa bongo fleva Zuhura Masoud 'Zuchu' kuendesha shughuli zozote za kisanaa visiwani humo vilevile imepiga marufuku vituo vya redio na TV kucheza kazi zake kwa kipindi cha miezi 6

account_circle
Tanzania Updates ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ(@TanzaniaUpdates) 's Twitter Profile Photo

Serikali nchini Ufaransa ya rais, Emmanuel Macron imeidhinisha sheria ya utoaji mimba kuwa haki ya kikatiba kwa wanawake ambapo watakuwa huru kufanya hivyo pindi wanapojisikia

account_circle
Tanzania Updates ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ(@TanzaniaUpdates) 's Twitter Profile Photo

Serikali kupitia naibu waziri wa mambo ya ndani Jumanne Sagini imetoa siku 14 kuondolewa kwa namba za 3D kwenye magari kwani namba hizo hazitengezwi na wakala mwenye kibali kutoka TBS na pia herufi hizo zina ugumu wa kusomeka katika umbali usiopungu mita 100

account_circle
Tanzania Updates ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ(@TanzaniaUpdates) 's Twitter Profile Photo

EPL : Klabu ya Arsenal imeibuka na ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Sheffield United ugenini usiku wa kuamkia leo

Arsenal bado imesalia nafasi ya 3 wakiwa na alama 61 nyuma ya Manchester City na vinara Liverpool kwa tofauti ya alama 2

account_circle
Tanzania Updates ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ(@TanzaniaUpdates) 's Twitter Profile Photo

Nchini Senegal mamia ya waandamanaji wameripotiwa kuendelea kumtaka rais wa nchi hiyo MackSall kufanya uchaguzi mkuu mwezi mmoja kabla ya muda wa urais wake kuisha April 2, 2024

account_circle
Tanzania Updates ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ(@TanzaniaUpdates) 's Twitter Profile Photo

Waziri wa afya Ummy Mwalimu amepiga marufuku vituo binafsi kuwaondoa wodini wagonjwa ambao ni wanachama wa NHIF mara baada ya saa 48 kupita kutolewa kwa taarifa hiyo na vituo hivyo.

account_circle
Tanzania Updates ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ(@TanzaniaUpdates) 's Twitter Profile Photo

Kupitia instagram stori mwanamuziki Wizkid ametudokeza juu ya ujio wa albamu yake mpya ikiwa ni miaka miwili tangu alipoachia albamu yake ya 'More Love, Less Ego'

account_circle
Tanzania Updates ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ(@TanzaniaUpdates) 's Twitter Profile Photo

TANZIA: Rais mstaafu awamu ya pili, Ally Hassan Mwinyi amefariki dunia hospitali jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa saratani ya mapafu

Mwinyi anatarajiwa kuagwa leo saa 8 mchana uwanja wa uhuru

account_circle
Tanzania Updates ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ(@TanzaniaUpdates) 's Twitter Profile Photo

Kiungo wa Juventus, Paul Pogba amefungiwa kujihusisha na soka kwa kipindi cha mjaka minne baada ya kugundulika anatumia dawa za kusisimua misuli, kufuatia vipimo vilivyofanyika Agosti 2023

account_circle
Tanzania Updates ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ(@TanzaniaUpdates) 's Twitter Profile Photo

Washukiwa 5 kati ya 6 wanaohisiwa kuhusika na mauaji ya rapper Kiernan Forbes maarufu kama 'AKA' wamefikishwa katika mahakama ya mkazi jijini Durban hii leo kujibu mashtaka

account_circle
Tanzania Updates ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ(@TanzaniaUpdates) 's Twitter Profile Photo

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa vyama vya siasa viendlee kufanya shughuli zao kwa uhuru huku akisisitiza kuwa wanaotaka kuandamana wanaruhusiwa na watalindwa

account_circle