Ahmada Salum (@ahmadasalum) 's Twitter Profile
Ahmada Salum

@ahmadasalum

🔗 @YALIRLCEA Alumni | Community Programs | Youth Advocate | Diplomat | National Chairperson @uncpamoja | SDGs Champion to the @unitednationstz

ID: 878419853685776384

calendar_today24-06-2017 01:09:48

669 Tweet

247 Takipçi

260 Takip Edilen

Ahmada Salum (@ahmadasalum) 's Twitter Profile Photo

"Hakuna mtu anayezaliwa akiwa na Chuki dhidi ya mwingine. Watu wanajifunza kuchukia, na Kama wanajifunza kuchukia maana yake pia wanaweza kujifunza Kupenda. Kwa maana Upendo unakuja kirahisi zaidi kwenye Mioyo ya watu kuliko Chuki" -Nelson Rolihlahla Mandela

Ahmada Salum (@ahmadasalum) 's Twitter Profile Photo

Tumekuja Duniani hatuna, tutaondoka hatuna. Siha njema ni tajamala, kuishi pia ni tajamala. Ukiangaza kwa kina katika ulimwengu hakuna kitu tunachomiliki, vyote tutaviacha siku ya kuondoka katika Mgongo wa Ardhi. Tusafishe mioyo yetu, ukiwa nacho kidogo shukuru, Ukikosa shukuru

Ahmada Salum (@ahmadasalum) 's Twitter Profile Photo

Wacha nipige nduru kidogo kwenu wana cholechole wenza Miaka na Mikaka ninayoendelea kuishi nimejifunza, Ngwe ili iwe ndogo uipimapo chutama, unapolitazama tatizo saaana utaingia uvivu, mavune na machuke kabla hujaanza kutatua Jikadirie, kulitazama tatizo ndio mwanzo wa matatizo

Ahmada Salum (@ahmadasalum) 's Twitter Profile Photo

Ni Makosa ya Ulimi yatakufanya uingie Motoni. Sisi tunaweza kuyaona ya kawaida lakini Kwa Mungu ni Makubwa sana. Si ustarabu kutoa matusi, kumsengenya mtu ambalo akisikia ataudhika, kumchongea mtu pahala ambapo atapata matatizo, kumfitini mtu mpaka akakosana na watu wanaoelewana

Ahmada Salum (@ahmadasalum) 's Twitter Profile Photo

#SikilizaAHMADA Ukimchukia Mtu haimaanishi kwamba M|Mungu hatoendelea Kumbariki, Maana Baraka za M|Mungu haziendeshwi na Chuki zako. Kila Mtu kwa KARAMA yake, KADRI yake na KUDRA yake! #Jikadirie

Ahmada Salum (@ahmadasalum) 's Twitter Profile Photo

#SikilizaAHMADA Mbaya wako ni mzuri kwa mwengine na mwema wako ni mbaya kwa mwengine. Ukipenda weka kiasi na ukichukia weka kiasi, inaweza kufika siku mbaya wako akawa mwema na mwema wako akawa mbaya. Zaidi; Tusitengeneze maadui kwa Stori za kuambiwa. #Jikadirie

Ahmada Salum (@ahmadasalum) 's Twitter Profile Photo

#SikilizaAHMADA Jitahidi sana starehe za siku ya mwaka mpya zisikusahaulishe hali na matatizo ya nyumbani kwenu. Aidha zisikutoe kwenye Utu wako na kupoteza heshima yako. Kuna maisha na familia baada ya Usiku wa Mwaka Mpya. #Jikadirie

Ahmada Salum (@ahmadasalum) 's Twitter Profile Photo

Katika masuala au majambo yanayoturudisha nyuma sana vijana wenzangu ni CHOYO katika Nyoyo zetu. Ni kutomtakia Zuri mwenzako, tunatafuta nafasi ya pale wakati gani atakosea na aoneoane hama maana mbele za watu. #Tukadiriane

Ahmada Salum (@ahmadasalum) 's Twitter Profile Photo

Tatizo ni pale tunapouliziwa taarifa zetu kwa watu wasiotupenda ndo watuelezee mahala ambapo hatuwezi kufika au kujitetea. Huo ni wakati mgumu na mbaya sana kwetu na ni wakati mzuri, sahihi na mujarabu sana kwao kutubomoa. Hiyo vita ushindi wake ni M|Mungu kuingilia kati.

Ahmada Salum (@ahmadasalum) 's Twitter Profile Photo

ISAYA [41:10] Basi,usiogope, mimi nipo pamoja nawe, usifadhaike, mimi ni Mungu wako nitakuimarisha na kukusaidia, nitakulinda kwa mkono wangu wa ushindi.